Models: 140000

Maelezo Jumla

Mwongozo huu una maelezo ya kiusalama kuhusu hatari zinazohusiana na injini na jinsi ya kuzizuia. Pia ina maagizo ya uendeshaji na udumishaji sahihi wa injini hii. Ni muhimu kwamba usome, uelewa, na ufuate maagizo haya.
Hifadhi mwongozo huu kwa ajili ya marejeleo ya siku zijazo.
Vielelezo na mifano iliyo katika mwongozo huu ni ya kimaelezo pekee na huenda ikatofautiana na muundo wako. Fuata vielelezo vinavyolingana na jinsi injini yako imefanyiwa usanidi. Ikiwa inahitajika, zungumza na Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa.
Rekodi tarehe ya kununua, muundo, aina, na nambari za msimbo za injini kwa ajili ya vipuri. Nambari hizi zipo kwenye injini yako. Rejelea sehemu ya
Vipengele na Vidhibiti
.
Tarehe ya Ununuzi
Muundo wa Injini - Aina - Msimbo
Nambari Tambulishi ya Injini

Maelezo ya Mawasiliano ya Ofisi ya Ulaya

Maelezo ya Mawasiliano ya Ofisi ya Ulaya
Ukiwa na maswali kuhusiana na mafukizo ya Ulaya, wasiliana na ofisi yetu ya Ulaya kupitia:
Max-Born-Straße 2, 68519 Viernheim, Germany.
 

Umoja wa Ulaya (EU) Awamu ya V (5): Viwango vya Kaboni Dioksidi (CO2)

Andika CO2 ndani ya upau wa kutafuta kwenye BriggsandStratton.com ili kupata viwango vya kaboni dioksidi vya injini za Briggs & Stratton zilizoidhinishwa za Aina ya EU. 

Usalama wa Mwendeshaji

Ishara ya Tahadhari ya Usalama na Maneno ya Ishara

Alama ya tahadhari ya kiusalama ya inatambulisha maelezo ya usalama kuhusu hatari zinazoweza kusababisha jeraha la kibinafsi. Neno la ishara (
HATARI
,
ONYO
, au
TAHADHARI
) linatumika kuonyesha uwezekano wa kujeruhiwa na ubaya wa jeraha hilo. Kwa kuongezea, alama ya hatari inatumika kuwakilisha aina ya hatari.
HATARI
inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa,
itasababisha
kifo au jeraha mbaya sana.
ONYO
inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa,
inaweza
kusababisha kifo au jeraha mbaya sana.
TAHADHARI
inaonyesha hatari ambayo, isipoepukwa,
inaweza
kusababisha jeraha dogo au wastani.
ILANI
inaonyesha maelezo yanayozingatiwa kuwa muhimu, lakini hayahusiani na hatari.

Habari Zinazohusiana

Usalama wa Mwendeshaji


Alama za Hatari na Maana Yake

Maelezo ya usalama kuhusu hatari zinazoweza kusababisha jeraha la kibinafsi.
Soma na uelewe Mwongozo wa Mwendeshaji kabla ya kutumia kifaa au kukifanyia huduma.
Hatari ya Moto
Hatari ya Mlipuko
Hatari ya Mshtuko
Hatari ya Moshi wenye Sumu
Hatari ya Maeneo Moto
Hatari ya Kuvutwa Nyuma kwa Haraka
Hatari ya Kukatwa Viungo - Sehemu Zinazosonga
Kiwango cha Mafuta - Upeo
Usijaze Kupita Kiasi

Habari Zinazohusiana

Usalama wa Mwendeshaji


Ujumbe wa Usalama

Injini za Briggs & Stratton® hazijaundwa kuzalisha nguvu za umeme au kuendesha: vijigari vya kufurahia; vijigari vya kuendesha; vya watoto, burudani, au magari ya barabara ya aina yote (ATV); pikipiki; gari la kuendeshea juu ya maji; bidhaa za ndege; au magari yaliyotumiwa katika matukio ya mashindano yasiyowekewa vikwazo na Briggs & Stratton. Kwa maelezo kuhusu bidhaa za mashindano ya uendeshaji magari, tazama www.briggsracing.com. Kwa matumizi pamoja na vifaa na ATV za upande kwa upande, tafadhali wasiliana na Kituo cha Matumizi ya Injini cha Briggs & Stratton, 1-866-927-3349. Matumizi ya injini isivyofaa inaweza kusababisha majeraha mabaya au kifo.

Habari Zinazohusiana

Usalama wa Mwendeshaji


Utumiaji tena wa Taarifa

Tumia tena mifuko yote, maboksi, oili na betri zilizotumika kama ilivyobainishwa na kanuni za serikali.

Vipengele na Vidhibiti

Vidhibiti vya Injini

Rejelea Vielelezo: Figure 1, Figure 2, Figure 3, na Figure 4 ili kujua maeneo ya vipengele na vidhibiti.
  1. Nambari Tambulishi za Injini
    Muundo - Aina - Trimu
  2. Plagi ya Spaki
  3. Tangi na Kifuniko cha Mafuta
  4. Kisafishaji Hewa
  5. Sehemu ya Kushika ya Kamba ya Kianzishaji
  6. Kifaa cha Kupima Oili
  7. Mafla, Kilinda Mafla (iwapo kipo), Kishika Spaki (iwapo kipo)
  8. Kifuniko cha Chumba cha Blowa
  9. Kidhibiti Injini (iwapo kipo)
  10. Choki (iwapo ipo)
  11. Vali ya Kufungia Mafuta (iwapo ipo)
  12. Swichi ya Kuzima (iwapo ipo)
  13. Prima (iwapo ipo)
Vidhibiti vya Injini 1
Vidhibiti vya Injini 2
Vidhibiti vya Injini 3
Vidhibiti vya Injini 4

Habari Zinazohusiana

Vipengele na Vidhibiti


Ishara za Kudhibiti Injini na Maana

Kasi ya Injini - HARAKA
Kasi ya Injini - POLEPOLE
Kasi ya Injini - SIMAMA
WASHA - ZIMA
Kuwasha Injini
Choki IMEFUNGWA
Kuwasha Injini
Choki IMEFUNGULIWA
Kifuniko cha Mafuta
Kizima Mafuta - KIMEFUNGULIWA
Kizima Mafuta - KIMEFUNGWA

Habari Zinazohusiana

Vipengele na Vidhibiti


Uendeshaji

Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Ukinusa gesi
  • Usiwashe injini.
  • Usiwashe swichi za kiumeme.
  • Usitumie simu katika eneo hilo.
  • Ondoka kwenye eneo hilo.
  • Wasiliana na idara ya wazima moto.
Unapoendesha kifaa
  • Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Unapohamisha kifaa hadi eneo nyingine
  • Hakikisha kwamba tangi la mafuta ni TUPU au kwamba vali ya kufunga mafuta ipo katika eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.

Mapendekezo ya Oili

Kiwango cha Oili
: Rejelea sehemu ya
Vipimo
.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
®
 ili kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinaruhusiwa ikiwa zimebainishwa kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa. Injini kwenye vifaa vingi vya kutumiwa nje zinafanya kazi vyema zikitumia oili ya 5W-30 Synthetic. Kwa vifaa vinavyoendeshwa katika joto la juu, oili ya Vanguard
®
15W-50 Synthetic inatoa ulindaji bora.
A
SAE 30 -
Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa kuwasha.
B
10W-30 -
Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi.
C
5W-30
D
Sinthetiki 5W-30
E
Vanguard
®
 Synthetic 15W-50

Habari Zinazohusiana

Uendeshaji


Kagua Kiwango cha Oili

Kabla ya kukagua au kuongeza oili
  • Hakikisha injini inadumisha mizani.
  • Safisha vifusi kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
  • Rejelea sehemu ya
    Vipimo
    ili kujua kiwango cha oili.
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza, hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi kukarabatiwa chini ya waranti.
  1. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1) na upanguze kwa kitambaa safi.
    Kagua Oili
  2. Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1).
  3. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo Figure 1) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili.
  4. Iwapo kiwango cha oili kiko chini, polepole weka oili kwenye eneo la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo Figure 1). Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
  5. Subiri dakika moja na ukague tena kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango cha oili ni sahihi.
  6. Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1).

Habari Zinazohusiana

Uendeshaji


Mapendekezo ya Mafuta

Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
  • Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
  • Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87/AKI 87 (91 RON). Matumizi katika mwinuko wa juu, tazama hapa chini.
  • Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inaruhusiwa.
Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Matumizi ya mafuta ambayo hayajaidhinishwa yataharibu vipengele vya injini, na haitakarabatiwa chini ya waranti.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi, na ubabuzi, changanya kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli ndani ya mafuta. Rejelea sehemu ya
Uhifadhi
. Mafuta yote si sawa. Iwapo matatizo ya kuwasha au utendakazi yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini za kabureta ni EM (Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)). Mifumo ya kudhibiti mafukizo kwa injini zilizo na unyonyaji mafuta kielektroniki ni ECM (Engine Control Module [Moduli ya Kidhibiti Injini]), MFI (Multi Port Fuel Injection [Unyonyaji Mafuta kwa Matundu Kadhaa]), TBI (Throttle Body Fuel Injection [Unyonyaji Mafuta kwa Kifaa cha Kuingiza Hewa]) na ikiwa ina O2S (Oxygen Sensor [Sensa ya Oksijeni]).

Mwinuko wa Juu

Katika minuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1524), kiwango cha chini cha okteni 85 / AKI 85 (RON 89) cha petroli kinakubalika.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha utendakazi. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka kwa utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko wa juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya fiti 2,500 (mita 762) na marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika.

Habari Zinazohusiana

Uendeshaji


Ongeza Mafuta

Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
  • Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili kuhakikisha injini imepoa.
  • Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
  • Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
  • Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine vya mwako.
  • Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
  • Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
  1. Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi. Ondoa kifuniko cha fueli.
  2. Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo Ongeza Mafuta) kwa mafuta. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta, usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta (B).
  3. Weka kifuniko cha mafuta.
    Ongeza Mafuta

Washa Injini

HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii, nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
  • Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali na madirisha, milango na matundu.
  • Sakinisha ving’ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji. Ving’ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
  • USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi, ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
  • KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
  • Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
  • Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
  • Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
  • Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
  • Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za kuwasha.
Sehemu zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, miguu, nywele, nguo, au vifuasi na kupelekea kukatwa viungo au ngozi vibaya.
  • Endesha kifaa vilinzi vikiwa vimesakinishwa vizuri.
  • Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
  • Vua vipuli na uhakikishe kwamba nywele ndefu ziko mbali na sehemu zinazozunguka.
  • Usivae nguo zilizolegea au vipengee vinavyoweza kushikwa.
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
  • Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
  • kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
  • Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi, vimeambatishwe salama.

Aina za Mfumo wa Kuwasha

Kabla ya kuwasha injini, ni lazima ujue aina ya mfumo wa kuwasha ambao uko kwenye injini yako. Injini yako ina mojawapo ya aina zifuatazo za mifumo ya kuwasha:
  • ReadyStart
    ®
    na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1:
    Mfumo wa kuwasha wa aina hii una choki otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina prima.
  • Mfumo wa Choki:
    Mfumo wa aina hii una choki ya kutumiwa katika mazingira yenye baridi. Baadhi ya miundo ina kidhibiti cha choki tofauti huku miundo mingine ina muunganiko wa choki na kidhibiti injini. Haina prima.
  • Mfumo wa Prima:
    Mfumo huu wa kuwasha una prima nayotumiwa kuwasha katika mazingira yenye baridi. Haina choki kikuli.
Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.

Choki, ReadyStart
®
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1

  1. Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya
    Kagua Kiwango cha Oili
    .
  2. Zima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
  3. Sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha FUNGUA
    Washa Injini
  4. Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
  5. Sogeza kidhibiti cha choki (F, Kielelezo Figure 2), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
  6. Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo Figure 2), iwapo ipo, hadi kwenye eneo linaloonyesha WASHA.
    Washa Injini 2
  7. Shikilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo, dhidi ya kishikio.
  8. Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (G, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo. Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji (G) polepole hadi uhisi ugumu, kisha vuta kwa haraka.
  9. Injini inapochemka, sogeza kidhibiti choki (F, Kilelelezo Figure 2) hadi eneo linaloonyesha FUNGUA.
    Injini ikikosa kuwasha, nenda kwenye au upige simu kwa nambari
    1-800-444-7774
    (nchini Marekani).

Habari Zinazohusiana

Washa Injini

Mfumo wa Prima

  1. Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya
    Kagua Kiwango cha Oili
    .
  2. Hakikisha kwamba umezima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
  3. Sukuma swichi ya kuzima (A, Kielelezo Figure 1), iwapo ipo, hadi kwenye eneo linaloonyesha WASHA.
    Mfumo wa Prima
  4. Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
  5. Sukuma kitufe cha prima nyekundu (F, Kielelezo Figure 1), mara tatu.
    Prima haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
    Ukibonyeza kitufe cha prima mara nyingi sana, injini itafurika na itakuwa gumu kuiwasha.
  6. Shikilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo, dhidi ya kishikio.
  7. Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (D, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo. Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi ugumu, kisha vuta kwa haraka.

Habari Zinazohusiana

Washa Injini


Zima Injini

Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
  • Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
  1. Achilia wenzo wa kuzima injini, iwapo upo.
  2. Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo Figure 2), iwapo ipo, hadi kwenye eneo linaloonyesha ZIMA.
  3. Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha SIMAMA.
  4. Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo Figure 1), iwapo ipo, hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.

Udumishaji

Maelezo ya Udumishaji

Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshtuko wa umeme, moto au mlipuko na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
  • Tenganisha nyaya zote za plagi ya spaki na uziweke mbali na plagi za spaki.
  • Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme).
  • Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
  • Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
  • Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha majeraha.
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kutengeneza injini hii ni lazima visalie kwenye maeneo yake ili kupata uendeshaji bora.
Mwone Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata huduma zote za udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za injini.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji


Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo

Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini.
Hata hivyo, ili kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya “bila malipo”, ni lazima kazi ifanywe na muuzaji aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji


Ratiba ya Udumishaji

Saa 5 za Kwanza
  • Badilisha oili ya injini (haihitajiki kwenye miundo iliyo na lebo ya
    Just Check & Add
    na
    Hakuna Kubadilisha Oili
    ).
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
  • Kagua kiwango cha oili ya injini.
  • Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
  • Safisha grili ya kuingiza hewa.
Kila Baada ya Saa 25 au Kila mwaka
  • Safisha chujio la hewa
    1
    .
  • Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
    1
    .
Kila Baada ya Saa 50 au Kila mwaka
  • Badilisha oili ya injini (haihitajiki kwenye miundo iliyo na lebo ya
    Just Check & Add
    na
    Hakuna Kubadilisha Oili
    ).
Kila Mwaka
  • Badilisha plagi ya/za spaki.
  • Badilisha chujio la hewa.
  • Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo).
  • Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
    1
    .
  • Kagua uwazi wa vali
    2
    .
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi hewani.
2
Haihitajiki isipokuwa kutokee matatizo ya utendakazi wa injini.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji


Kabureta na Kasi ya Injini

Usihitilafiane na kabureta, springi ya kidhibiti, viunganishaji, au sehemu nyingine ili kubadilisha kasi ya injini. Iwapo marekebisho yoyote yanahitajika, wasiliana na Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kufanyiwa huduma.
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama ilivyosakinishwa kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu zaidi ya kifaa hiki ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa oparesheni salama na sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa na mtaalamu wa huduma aliyehitimu.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji


Kufanyia Huduma Ekzosi na Mifumo ya Kupoesha

Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto, unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika moto.
  • Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
  • Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia mtiririko wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana. Hii inapelekea utendakazi usioridhisha na kufupisha maisha ya injini. Mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kuwa na vifusi ambavyo haviwezi kuondolewa bila kufungua baadhi ya shemu za injini. Hakikisha kwamba Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton amekagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa. Rejelea
Ratiba ya Udumishaji
.
  1. Hakikisha kwamba hakuna vitu vinavyoweza kushika moto karibu na nyuma ya mafla.
  2. Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye maeneo ya kifuniko cha chumba cha blowa, mafla na silinda. USITUMIE maji kusafisha injini.
  3. Hakikisha viunganishaji, springi na vidhibiti ni safi.
  4. Kagua mafla kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine.
  5. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Hakikisha kwamba unasafisha au kusakinisha vipuri kabla ya kuendesha kifaa.
  6. Ikiwa yapo, hakikisha mapezi ya kupoesha oili ni safi.

Kufanyia Huduma Plagi ya Spaki


Kagua pengo la plagi ya spaki (A, Kielelezo Pengo la Plagi ya Spaki) ukitumia pamba ya waya (B). Ikiwa inahitajika, rekebisha pengo la plagi ya spaki.  Sakinisha na ukaze plagi ya spaki kwa kiwango sahihi. Ili kupata maelezo maalum ya pengo na kukaza, rejelea sehemu ya
Maelezo
.
Pengo la Plagi ya Spaki

Habari Zinazohusiana

Udumishaji


Badilisha Oili ya Injini

Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto, unaweza kuchomeka.
  • Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
  • Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Kwa miundo ya
Just Check & Add
, hauhitaji kubadilisha oili. Ikiwa unahitaji kubadilisha oili, basi fuata utaratibu ufuatao.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji

Ondoa Oili

  1. Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D, Kielelezo Figure 1) na uiweke mbali na plagi ya/za spaki (E).
    Ondoa Waya wa Plagi ya Spaki
  2. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 2).
    Badilisha Oili
  3. Wakati unamwaga oili kutoka kwenye mrija wa kujazia oili wa upande wa juu (C, Kielelezo Figure 3), weka upande wa injini ulio na plagi ya spaki (E) ukiwa umeangalia juu. Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
    Mrija wa Kumwaga Oili

Habari Zinazohusiana

Badilisha Oili ya Injini

Ongeza Oili

  • Hakikisha injini inadumisha mizani.
  • Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
  • Rejelea sehemu ya
    Vipimo
    ili kujua kiwango cha oili.
  1. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1). Futa oili kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
  2. Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo Figure 1).
    Usijaze kupita kiasi.
      Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
  3. Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1).
  4. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo Figure 1) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili.
  5. Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo Figure 1).
  6. Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu ya 
    Kuondoa Oili
    .

Habari Zinazohusiana

Badilisha Oili ya Injini


Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa

Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
  • Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama
Ratiba ya Udumishaji
ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.

Habari Zinazohusiana

Udumishaji

Kichujio cha Povu la Hewa

  1. Legeza au uondoe vifaa vya kufunga (A, Kielelezo Figure 1), iwapo vipo.
  2. Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo Figure 1).
  3. Kwa uangalifu ondoa elementi ya povu (C, Kielelezo Figure 1) kutoka kwenye sehemu ya chini ya chujio la hewa.
  4. Osha elementi ya povu (C, Kielelezo Figure 1) kwenye sabuni oevu na maji. Finya elementi ya povu ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu mpaka ikauke.
  5. Tumbukiza elementi ya povu (C, Kielelezo Figure 1) ndani ya oili safi ya injini. Ili kuondoa oili ya injini isiyohitajika kwenye elementi ya povu, ifinye ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu.
  6. Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo Figure 1) kwenye sehemu ya chini ya chujio la hewa.
  7. Funga au weka kifuniko (B, Kielelezo Figure 1) na ufunge vizuri ukitumia bizimu. Hakikisha kwamba umekaza vizuri.
    Chujio la Hewa la Povu

Habari Zinazohusiana

Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa

Kichujio cha Hewa cha Karatasi


  1. Ondoa kifuniko (B, Kielelezo Figure 1).
    Kichujio cha Hewa cha Karatasi
  2. Ondoa chujio (C, Kielelezo Figure 1).
  3. Ondoa kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, kwenye chujio (C).
  4. Ili kuondoa uchafu usiotakikana kwa utaratibu gongesha chujio kwenye eneo gumu. Ikiwa chujio ni chafu libadilishe kwa chujio jipya.
  5. Osha kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo Figure 1), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu na maji. Acha kisafishaji cha mwanzo kikauke kabisa.
    Usiongeze
    oili kwenye kisafishaji cha mwanzo.
  6. Funga kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo Figure 1) kilichokauka, ikiwa kipo, kwenye chujio (C).
  7. Sakinisha chujio (C, Kielelezo Figure 1).
  8. Sakinisha kifuniko (B, Kielelezo Figure 1).

Habari Zinazohusiana

Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa


Hifadhi

Mfumo wa Mafuta

Mfumo wa Mafuta-Mow-Stow
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana. Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
  • Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
Miundo mingine ina tangi la mafuta la uhifadhi wima ambao unaruhusu injini kuinama kwa ajili ya udumishaji au uhifadhi (C, Kielelezo Figure 1). Usihifadhi ikiwa wima wakati tangi la mafuta limejaa kupita kiwango cha alama ya kiwango cha mafuta (D), iwapo ipo. Kwa maagizo zaidi, rejelea mwongozo wa kifaa.
Weka injini bila kuinama (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo Figure 1) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuganda yanapohifadhiwa kwenye kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya siku 30. Inapendekezwa kutumia kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli kwenye kontena ya kuhifadhi mafuta. Hii inafanya mafuta kukaa yakiwa safi na kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo wa mafuta.
Unapojaza kontena hiyo ya mafuta kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta bila alcoholi kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtenegenzaji. Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi mafuta yaishe.
Uhifadhi Ikiwa Wima

Habari Zinazohusiana

Hifadhi


Oili ya Injini

Wakati injini bado ina joto, badilisha oili ya injini. Rejelea sehemu ya
Kubadilisha Oili ya Injini
.

Habari Zinazohusiana

Hifadhi


Kutatua Matatizo

Usaidizi

Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda kwenye au piga simu kwa nambari
1-800-444-7774
(nchini Marekani).

Habari Zinazohusiana

Kutatua Matatizo


Maelezo na Sehemu za Udumishaji

Vipimo Maalum
Modeli:
080000
Modeli:
090000
Unyonyaji Mafuta
7.63
ci (
125
cc)
8.64
ci (
140
cc)
Shimo
2.362
in (
60
mm)
2.495
in (
63,4
mm)
Mpigo
1.75
in (
44,45
mm)
1.75
in (
44,45
mm)
Kiwango cha Oili
15
oz (
,44
L)
15
oz (
,44
L)
Pengo la Plagi ya Spaki
.020
in (
,51
mm)
.020
in (
,51
mm)
Mkufu wa Plagi ya Spaki
180
lb-in (
20
Nm)
180
lb-in (
20
Nm)
Pengo la Hewa
.006 - .014
in
(
,15 - ,36
mm)
.006 - .014
in
(
,15 - ,36
mm)
Mwanya wa Vali ya Kuingiza Hewa
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
Mwanya wa Vali ya Ekzosi
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
Vipimo Maalum
Modeli:
093J00
Modeli:
100000
Unyonyaji Mafuta
9.15
ci (
150
cc)
9.93
ci (
163
cc)
Shimo
2.583
in (
65,60
mm)
2.688
in (
68,28
mm)
Mpigo
1.75
in (
44,45
mm)
1.75
in (
44,45
mm)
Kiwango cha Oili
15
oz (
,44
L)
15
oz (
,44
L)
Pengo la Plagi ya Spaki
.020
in (
,51
mm)
.030
in (
,76
mm)
Mkufu wa Plagi ya Spaki
180
lb-in (
20
Nm)
180
lb-in (
20
Nm)
Pengo la Hewa
.006 - .014
in
(
,15 - ,36
mm)
.006 - .014
in
(
,15 - ,36
mm)
Mwanya wa Vali ya Kuingiza Hewa
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
Mwanya wa Vali ya Ekzosi
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
.004 - .008
in
(
,10 - ,20
mm)
Vipuri
Ili kununua vipuri vya Briggs & Stratton, tafuta Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa kwenye .
 Utahitaji nambari yako ya utambulisho (muundo - aina - trimu). Rejelea kwenye sehemu ya
Vipengele na Udhibiti
ili kupata nambari ya utambulisho ya injini yako.

Vipimo vya Umeme

Kichwa kinaoonyeshwa. Taarifa ya kanusho la vipimo vya nishati iliidhinishwa mnamo 3/1/2013. Ya kutumiwa na miundo niliyo na injini za Briggs & Stratton*. ***Rekebisho A, hakuna mabadiliko. Imerekebishwa tu ili kuruhusu mtafsiri kupitia matini asili. 
Kipimo kamili cha umeme kwa miundo ya injini za petroli kimewekwa kulingana na SAE (Jamii ya Wahandisi wa Magari) msimbo J1940 Utaratibu wa Kipimo cha Umeme & Mkufu wa Injini Ndogo na umepimwa kulingana na SAEJ1995. Viwango vya mkufu vinafikia 2600 RPM kwa injini zenye “rpm” iliyowekwa kwenye lebo na 3060 RPM kwa injini zingine zote; viwango vya nguvu ya injini vinafikia 3600 RPM. Vizingo vya umeme kamili vinaweza kutazamwa katika www.BRIGGSandSTRATTON.COM. Viwango jumla vya umeme vinachukuliwa ekzosi na kisafishaji hewa zikiwa zimewekwa ilhali viwango vya umeme jumla vinachukuliwa bila vipengee hivi kuwekwa. Nguvu kamili halisi ya injini itakuwa juu zaidi kuliko nishati ya injini na yanaathiriwa na, miongoni mwa mambo mengine, hali iliyoko ya kuendesha na utofauti wa injini hadi nyingine. Kukiwa na bidhaa nyingi ambazo zimewekwa injini, injini ya petroli huenda ikakosa kufikia kadirio la nguvu kamili inapotumiwa katika kifaa cha umeme. Tofauti hii inatokana na vipengele mbalimbali zikijumuisha, lakini sio tu, vijenzi mbalimbali vya injini (kisafishaji cha hewa, ekzosi, kuchaji, upunguzaji halijoto, kabureta, pampu ya mafuta, n.k), vipimo vya matumizi, hali zilizoko za kuendesha (halijoto, unyevunyevu, mwinuko), na utofauti kati ya injini moja hadi injini nyingine. Kutokana na vipimo vya utengenezaji na uwezo, Briggs & Stratton wanaweza kuibadilisha injini hii kwa injini iliyo na nguvu nyingi zaidi. 

Habari Zinazohusiana

Maelezo na Sehemu za Udumishaji


Udhamini

Waranti ya Injini ya Briggs & Stratton
®

Kuanzia Agosti 2022

Hakikisho lenye Kipimo

Briggs & Stratton inatoa waranti kwamba, wakati wa kipindi cha waranti kilichobainishwa hapa chini, itafanyia ukarabati au kubadilisha, bila malipo, kwa kutumia sehemu mpya au iliyotengenezwa upya, kwa uamuzi wa Briggs & Stratton peekee, sehemu yoyote ambayo ina matatizo katika nyenzo au ufanyakazi au yote mawili. Gharama za usafirishaji bidhaa zilizowasilishwa ili kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa chini ya hakikisho hili ni lazima zigharimiwe na mnunuzi. Hakikisho hili linatumika na liko chini ya vipindi vya muda na masharti yaliyoelezwa hapa chini. Ili kupata huduma ya waranti, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye . Ni lazima mnunuzi awasiliane na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa, na kisha apeleke bidhaa kwa Muuzaji Huduma huyo Aliyeidhinishwa ili kufanyiwa ukaguzi na majaribio.
Hakuna hakikisho lingine la haraka. Waranti zilizoashiriwa, ikiwa ni pamoja na zile za uuzaji na uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, zina kipimo cha kipindi cha mwaka mmoja tangu kununuliwa, au kwa kiwango kilichoruhusiwa na sheria. Waranti nyingine zote zilizoashiriwa hazijumuishwi. Dhima ya uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo jingine haijajumuishwa kwa kiasi kinaruhusiwa na sheria.
Baadhi ya majimbo au nchi haziruhusu vipindi vya hakikisho kuwekewa vipimo, na baadhi ya majimbo au nchi haziruhusu kutojumuishwa au kipimo cha uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo jingine, kwa hivyo kipimo na kutojumuishwa huku huenda hakukuhusu wewe. Waranti hii hupeana haki maalum za kisheria na pia unaweza kuwa na haki nyingine ambazo zinatofautiana kulingana na jimbo na nchi
*
.
Masharti Wastani ya Udhamini
1, 2
Vanguard
®
; Msururu wa Kibiashara
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 36
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 36
Msururu wa XR
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 24
Injini Nyingine Zote Zenye Mkono wa Kalibu ya Chuma ya Dura-Bore™
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 12
Injini Nyingine Zote
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 3
1
Haya ni masharti yetu wastani ya waranti, lakini mara kwa mara huenda kukawa na vipengele vya ziada vinavyosimamiwa na waranti ambavyo havikusimamiwa wakati wa uchapishaji. Ili kupata orodha ya masharti ya sasa ya waranti ya injini yako, nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au uwasiliane na Muuzaji Huduma wako Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
2
Hakuna waranti kwa injini za vifaa vilivyotumiwa kutoa nishati badala ya kifaa kinachofaa; jenereta ya akiba kwa madhumuni ya kibiashara, magari ya kubebea mizigo yanayozidi kasi ya 25 MPH, au injini zinazotumiwa katika mashindano ya mbio au kwenye viwanja vya kibiashara au vya kukodishwa.
*
Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na waranti ambazo haziwezi kutojumuishwa chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa pesa kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku za usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo bidhaa hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa njia kubwa. Ili kupata huduma ya waranti, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye , au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au kwa kutuma barua pepe kwa salesenquiries@briggsandstratton.com.au, au kutuma barua kwa Briggs & Stratton Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank, NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha waranti huanzia tarehe ya ununuzi ya mtumiaji wa kwanza kununua dukani rejareja au mtumiaji wa mwisho wa kibiashara, na inaendelea kwa kipindi cha muda kilichobainishwa katika jedwali lililo hapa juu. “Matumizi ya kibinafsi” inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. “Matumizi ya kibiashara” inamaanisha matumizi mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha mapato au ya kukodisha. Pindi tu injini inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya hapo itazingatiwa kuwa injini ya matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili.
Usajili wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya waranti ya bidhaa za Briggs & Stratton. Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa tarehe ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya waranti inapoombwa, tarehe ya utengenezaji wa bidhaa itatumiwa kubaini kipindi cha waranti.

Kuhusu Hakikisho Lako

Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au utendakazi, na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho kina injini husika. Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au kuchakaa na kuchanika kwa kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile, hakikisho halitumiki ikiwa injini imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari tambulishi ya injini imeharibiwa ua kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu kwenye injini au matatizo ya utendakazi wa injini yanayosababishwa na:
  1. Matumizi ya sehemu ambazo si
    Briggs & Stratton
  2. Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi;
  3. Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa zaidi ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka au gesi asili kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo na
    Briggs & Stratton
    kuendeshwa kwa mafuta kama hayo;
  4. Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya;
  5. Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela au vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo au ukazaji wa v-belt kupita kiasi;
  6. Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk., ambavyo havijatolewa na
    Briggs & Stratton
    ;
  7. Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota vya panya vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la kuongeza kasi, au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha;
  8. Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua kukata au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji vibaya wa vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo;
  9. Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji, ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya.
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa
Briggs & Stratton
. Tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye au kwa kupiga simu kwa nambari 
1-800-444-7774
(nchini Marekani).

80114782 (Rekebisho A)

Habari Zinazohusiana

Udhamini


Back to Top